Home » Korti Yasimamisha Ujenzi Wa Soko Kitengela
News

Korti Yasimamisha Ujenzi Wa Soko Kitengela

Na Robert Masai, Kajiado Mjini.

Wafanyibiashara mjini Kitengela wamepata afueni ya muda baada ya mahakama ya Kajiado kuamru serikali ya kaunti kutohitilafia shuguli zao hadi pale kesi Iliyowasilishwa mahakamani itasikiliswa.

Akitoa amri hiyo kwenye kesi iliyowasilishwa mapema leo na Joseph Kinyanjui akitaka ishugulikiwe kwa dharura kwa niaba ya wafanyibiashara hao waliotaka kuzuia serikali ya kaunti kutekeleza notisi iliyotarajiwa kukamilka tarehe 26 mwezi huu.

 Hakimu wa Mahakama hiyo, Margaret Kasera amemuru serikali ya Kaunti kusitisha mipango yake ya kuwaondoa wafanyibiashara hao katika soko la Kitengela hadi pale kesi hiyo itakaposikiswa na kuamuliwa Mei 29, mwaka huu.

Kumekuwa na vuta nikuvute baina ya wafanyibishara mjini Kitengela kuhusu mpango wa serikali ya kaunti hiyo ya kutaka kuwaondoa sokoni humo kwa muda na kuwahamishia katika sehemu mbdala ili watoe nafasi ya soko hilo likarabatiwe.

Mpango huo uliopingwa vikali na waafanyibiashara hao, wakilaumu seriklai ya Kaunti kwa kutowapa sikio kabla ya kuchukua hatua ya kuwahamisha.

Comments

comments

Add Comment

Click here to post a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

%d bloggers like this: